JARIDA LA ATD DUNIA YA NNE TANZANIA – Aprili 2017

Wapendwa marafiki,
Ni tumaini langu kwamba nyote hamjambo. Katika chapisho hili
ninayo furaha kuwaleteeni habari za mafanikio kuhusu shule za
msingi, mkutano mkuu wa Dakar, Senegal na kampeni ya
uhamasishji ya ATD 2017.

Ninao uhakika kwamba mnakumbuka chapisho la mwezi wa July 2016, tulipotoa mapendekezo kumi na matano yaliyotokana na utafiti wa shule za msingi uliofanywa na wanachama wa ATD katika wilaya ya Kinondoni. Wanachama hao hao wakiwemo watu
wanaoishi katika umaskini uliokithiri, walimu na wafanyakazi wa kujitolea wa ATD, sasa wanafanya kazi ya kutetea mapendekezo hayo kwa wadau mbali mbali wa elimu, wazazi, viongozi wa serikali za mitaa na NGO zinazofanya kazi katika sekta ya elimu. Katika mikutano mitatu ya wazazi na walimu iliyofanyika katika shule za msingi msingi Pwani, Tandale na Melenia ya tatu washiriki zaidi ya 1,400 walihudhuria, mapendekezo yalipokelewa vizuri na
kusababisha mijadala yenye shauku kubwa kati ya walimu, wazazi,na kamati za shule. Kazi hii ya kutetea matokeo ya mapendekezo itaendelea katika mwaka wote wa 2017.

Chapisho hili linalenga hasa kukuletea kisa cha utashi wa familia moja katika kuzishinda changamoto na kutengeneza ushirikiano mpya uliojengwa katika uelewa na heshima, ukionesha jinsi mapendekezo ya Elimu kwa Wote yanavyoweza kuleta msukumo kwa uhalisia katika familia moja. Tangu 2016 hadi 2017 mchakato wa Mkutano Mkuu umekuwa ukifutiliwa katika kanda ya Afrika,
ukuhusisha 34 ya wanachama wa ATD. Mkusanyiko wa Dakar mwanzoni mwa mwezi March ulikuwa matokeo ya huu mchakato.

Ukurasa wa mwisho umetolewa kwa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa muasisi wa shirika la ATD Joseph Wresinski; miaka sitini ya kuanzishwa kwa shirika 1957 na miaka thelathini tangu siku ya Kutokomeza Umaskini Duniani ilipoadhimishwa mara ya kwanza tarehe 17 Oktoba 1987. Katika mwaka huu maalumu wanachama wa ATD watajitoa kikamilifu katika tamko la UMASKINI BASI: Wakiwepo watu kutoka duniani kote kuchukua hatua katika kuutokomeza umaskini,

Robert Jordan,
Timu ya Uongozi, ATD Dunia ya Nne, Tanzania.

Kuendelea kusoma jarida hili, download PDF.