Jarida la kwanza la mwaka 2021
Wapendwa marafiki wa ATD Dunia ya nne, ni matumaini yetu kuwa mpo salama huku mukiendelea na shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi ili kuhakikisha kuwa tunatokomeza umaskini mwezigoni mwetu.
Pia tunayofuraha kuwakaribisha kusoma jarida letu la kwanza kwa mwaka huu 2021, Katika jarida letu tutaeleza namna ambavyo janga la korona limeathiri jamii maskini na namna ambavyo tulishirikiana na kupambana kwa pamoja, maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini uliokithiri katika jamii ambayo yaliazimishwa tarehe 17, Oktoba, 2020, ambapo kauli mbiu ya siku hiyo ilikuwa ni “kuchukua hatua kwa pamoja ili kufikia haki za kijamii na mazingira kwa wote”.
Pia tutaeleza juu ya ukaribisho wa wageni ambao ni wafanya kazi wa kujitolea wa ATD Dunia ya nne na pia tulivyowaaga ndugu zetu Salma na Salehe ambao pia ni wafanyakazi wa kujitolea wa ATD Dunia ya nne ambao wamehamia mkoani Njombe kwa ajili ya majukumu ya harakati za kupambana na kutokomeza umaskini.
Mwisho kabisa ni ukurasa ambao utakuwa umesheheni picha za matukio mbalimbali.
Hayo ni yale ambayo kwa pamoja tuliweza kuyashuhudia na kuyatekeleza kwa mwaka 2020.
Tuungane kwa pamoja kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini uliokithiri katika jamii zetu.
Hamisi I. Matibu, mwanaharakati wa ATD dunia ya nne Tanzania.