MAREJEO YA 2016 – ATD Tanzania
UTAMBULISHO
Tunayo furaha kuwaletea taarifa ya matukio muhimu, masimulizi na
shughuri zilizotuhamasisha sote katika mwaka 2016.
Kupitia kwa wanachama, ATD Dunia ya Nne ilijikita kwa moyo, nguvu na juhudi katika kusaidia jamii kukabiliana na hali ya umaskini uliokithiri. Mwaka 2016 uliruhusu uhamasishaji wa nguvu wa wanachama wa ATD katika masuala mbalimbali ya elimu katika maeneo mbalimbali katika ukamilifu wake. Katika adhimisho la Siku ya Kutokomeza Umaskini Duniani, zaidi ya watu mia mbili walikusanyika ikiwa fursa kwa marafiki, familia na wanaharakati (watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri, wakichukua majukumu katika harakati za shirika) wafanyakazi wa kujitolea wa kudumu wakiwakilisha na kutoa taarifa kuhusu harakati za kidunia.
Marejeo haya ya mwaka yana lengo moja: kushirikishana nawe mtazamo wa kidunia wa watu husika na kukuonesha mitazamo mbalimbali ya mapambano dhidi ya umaskini uliokithiri yanayoongozwa na Shirika kupitia wanachama wake.
Mwaka 2017 tutaadhimisha pamoja miaka mia moja ya kuzaliwa
Joseph Wresinski, miaka 30 ya maadhimisho ya Siku ya Kutokomeza
Umaskini Duniani na miaka 60 ya kuanzishwa ATD Dunia ya Nne.
Tuzidi kuwa pamoja.