Tanzania 2015: Mwaka Katika Tathmini
Mwaka 2015 haujapita sana. Mapitio haya ni mwaliko wa
kukumbuka nyakati nzuri za nyuma za kushiriki, matukio,
kukutana na kila mwanachama wa ATD Dunia ya Nne kama
ilivyokuwa kwa mwaka uliopita.
Ni fursa ya kuweka wazi mafanikio yetu. Kwa mfano mwaka
uliopita tarehe 17 Oktoba, katika Siku ya Kimataifa ya
Kuushinda Umaskini Uliokithiri ambapo tulikuwa mamia kwa
mamia ya watu kuonesha lengo moja la kujitoa katika kuupiga
vita umaskini uliokithiri.
Watu wazima waliweza kuendelea katika kusoma na kuandika,
wazazi waliweza kupata vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wao ili
kuhakikisha wanapata nafasi ya kuwapeleka shuleni, kundi la
wanachama ATD Dunia ya Nne walishiriki katika utafiti mkubwa
kuhusu elimu.
Hata hivyo tunafahamu changamoto ambazo familia zinazoishi
katika umaskini uliokithiri wanakabiliana nazo lakini mafanikio
yote tuliyopata yanatoa matumaini kwa dunia ambapo kila mtu
anaweza kuishi kwa amani na heshima.