Tanzania jarida Agosti 2017
’’Hatuna budi kufanya kazi wote kwa pamoja ili kuhakikisha wale waanaoishi katika umasikini uliokithiri wanapata haki zao, sauti zao zinasikika na kuheshimiwa utu wao.’’.
Magdalena Sepulveda Carmona, Mwandishi wa makala yanayohusu umasikini uliokithiri na haki za bindamau kutoka umoja wa mataifa.
Kwa kusimama na kupaza sauti iwe katika mikutano ya jamii au katika vikao vya umoja wa mataifa kila mwanajumuiya wa ATD anasimama na kuwatetea watu wanaoishi katika umasikini uliokithiri. Msimamo huu unahitaji ujasiri.
Padre Mtakatifu Joseph, Mwanzilishi wa ATD Dunia ya nne alizungumzia kuhusu marafiki wa kwanza wa ATD’’Utu huu pengine mwanzoni walifikiri watajihusisha na programu za kawaida. Kwa kweli mwishoni walijikuta wanahatarisha uaminifu wao. Si tu walikuwa wanatetea idadi ya watu isiowezekana kutetewa lakini pia kupitia mipango yao walikua wakiyahukumu kimakosa mashirika ya misaada. Walikuwa na wasiwasi wa kuhatarisha uaminifu wao kwa hali hii wakiwa machoni pa watu wao wenyewe.
Katika jarida hili tutasikia mapendekezo ya mpango wa utetezi wa ATD elimu kwa wote. Timu ya elimu kwa wote imekutana na wadau wa elimu zaidi ya 1000 wakiwemo wazazi na Viongozi wa serikali za mitaa kwa pamoja waliwezesha majadiliano baina yao juu ya mada ya elimu kwa wote. Wanachama wa ATD pia walikutana na Afisa Elimu wa wilaya ya Ilala na alikubali kuongeza mapendekezo katika kazi yao.
Utafiti wa ’’kipimo cha umasikini’’ ulizinduliwa rasmi. Tunasikia kutoka kwa Bwana Kassian, mwanachana wa kamati ya Kitaifa ya utafiti inayoongoza mradi . Na mwisho kabisa Pelagie, rafiki mpya wa harakati hii akishirikiana mawazo yake katika kugundua ATD. Kila mtu katika jarida hili yuko tayari kutetea haki za wale wanaoishi katika umasikini uliokithiri, Kupaza sauti kupinga udhalimu, kuhatarisha undugu na urafiki mbele ya jamii na marafiki zao kwa ajili ya wale wale wanaoishi katika umasikini uliokithiri. Kuweka msimamo kwa lengo la mabadiliko ya jamii . Kwa kupitia kila mpango wanajenga harakati zetu.
Hamisi Mpana
Mwanaharakati wa kudumu wa ATD.