Tanzania Jarida Agosti 2018
Ndugu wapendwa,
Kama ilivyoonyeshwa katika jarida letu la hivi karibuni, mradi wetu wa utafiti unaoendelea juu ya umaskini (unaogusa nyanja mbali mbali), kupitia mikutano na mijadala na watu wanaoishi katika umaskini na wadau wengine, umeonyesha wazi kwamba, uhalisia wa kiwango cha umaskini uliokithiri unaweza kutazamwa katika sura na vipengele mbali mbali.
Mwezi wa sita mwaka huu, watoto ndio walikuwa kiini katika kazi za nje katika mradi huu. Kwa makubaliano maalum, walituelezea jinsi wanavyonyimwa haki zao za msingi kama kutokuwa na muda wa kutosha kufurahia utoto wao na changamoto za kupata elimu inavyoweza kuboresha uwezekano wao wa kutotambua uwezo wao wa kupambana na magumu katika maisha yao ya baadae wakishakuwa watu wazima.
Katika Mwezi wa sita, Watu wanne wawakilishi kutoka ATD Tanzania walishiriki katika semina ya kimataifa iliyofanyika makao makuu ya shirika la ATD Dunia ya Nne yaliyoko, Pierrelaye nchini Ufaransa, iliyohusisha washiriki kutoka nchi kumi na nne duniani. Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kubadilishana ujuzi na uzoefu wa ‘kujifunza kutoka katika mafanikio’ ili kuelewa kwa ufasaha mambo ya msingi kwa elimu yenye mafanikio kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na watoto wanaoishi katika umaskini uliokithiri. Tazama jinsi wawakilishi wetu walivyoshiriki.
Simulizi zenye kuleta mabadiliko, ni mpango wa ATD katika kampeni ya kutokomeza umaskini mwaka 2017, ilimshirikisha mwanachama mmoja kutoka ATD Dunia ya Nne Tanzania, Reuben. Simulizi ya Maisha yake, iliyoelezewa hapa, inaelezea jinsi watu wakiungana pamoja kupitia ushirikiano wa wanakijiji ulivyowawezesha jamii nzima kupata maendeleo.
Katika kuonyesha umuhimu wa elimu, Jarida letu lilishirikisha mpango wa watu wazima kupata fursa ya kujua kusoma na kuandika ulioandaliwa na ATD katika eneo la Tandale jijini Dar es Salaam na jinsi lilivyo wawezesha kundi la wanaojifunza kuibua vipaji vya kusoma na kuandika. Na matokeo yake, waliojifunza sasa wanajisikia kuwajasiri na huru, kwa kuweza kufanikiwa kupata hatua binafsi ya kuwawezesha kupambana na maisha ya kutengwa katika jamii na kuitokemeza kabisa hofu ya kunyanyasika.
Tunatumaini utafurahia kusoma Jarida letu.
Laurent Ganau, ATD Dunia ya Nne Tanzania.