Tanzania Jarida September 2019
Ndugu wapendwa,
Ni matumaini yangu kuwa ni wazima wa afya na mnaendelea vizuri katika harakati za mapambano dhidi ya umaskini uliokithiri. Nasi hapa ATD Dunia ya nne tunaendelea na harakati pamoja na kuhakikiksha shughuli zote zinaendelea tukianza na maadhimisho ya siku ya kutok- omeza umaskini uliokithiri duniani tarehe 17 Oktoba 2019 Kamati ya maandalizi inaen- delea na maandalizi ya maadhimisho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa chuo cha ufundi stadi cha Don Bosco kilichopo oyster- bay ikisindikizwa na kauli mbiu isemayo “kushirikiana kwa pamoja kuwezesha watoto, familia na jumuiya zao katika kutokomeza umaskini.” Pia tunaendelea na shughuli za maktaba ya mtaa, ambapo inaendelea kuwezeshwa na vijana wa ATD Dunia ya nne, katika kuboresha wawezeshaji wamekuja na wazo la kuwapeleka watoto maktaba ya taifa kwa ajili ya kujisomea. Hii inawafanya watoto kupenda kusoma vitabu na watoto wameipokea vizuri.
Baada ya kufanya utatifiti kwa miaka mitatu Kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, mradi huu wa kubaini vipimo vya umaskini ume- hitimishwa mwezi juni 2019 kwa kufanya kikao kikubwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya mawasilisho ya vipimo na kuitambulisha mbinu mpya ya utafiti ya kuunganisha maarifa (MoK). Pia kwa mwezi uliopita kulikua na matukio kadhaa ikiwemo semina ya vijana ililyofanyika nchini Rwanda iliyo- husu mafunzo ya Tapori. Huu ni mtandao wa mawasiliano wa watoto ambao huwaleta wa- toto pamoja na kubadilishana uzoefu na maarifa ya watoto kutoka sehemu mbalimbali duniani kote. Pia kulikua na semina iliyohusu masuala ya fedha, semina hi ilihusisha wafan- yakazi wawili wa kudumu wa ATD Dunia ya nne. Mafunzo hayo yameweza kuwajengea uwezo mkubwa katika utunzaji wa fedha na maadili yake.Vilevile vijana wawili walikwen- da kwenye semina huko makao makuu Ufa- ransa. Semina hiyo ilihusu mawasiliano, kama tunavyojua mawasiliano ni kitu muhimu kati- ka mwenendo wetu ili kujua taarifa kutoka makao makuu na kutoka katika maeneno mengine duniani kote.
Tumekuwa na upungufu wa wafanyakazi w kudumu wa ATD dunia ya nne hapa kwetu Tanzania baada ya wafanyakazi wawili ku- hamishiwa makao makuu Ufaransa, hili ni jambo la kawaida kiutendaji na lengo ni ku- kujifunza na kufanikisha shughuli za ATD Dunia ya nne.
Tunatumaini utafurahia kusoma jarida letu.
Venance F. Magombera