Tanzania June-August 2015 (Swahili)
FULL TEXT ATD Tanzania June-August 2015 SW
Editorial
Rafiki Mpendwa,
Tunafuraha kukutumia baadhi ya habari kutoka kwa wanachama wa ATD Dunia ya Nne. Tokea jarida letu la mwisho, tulipata fursa ya uzoefu katika matukio mbalimbali ambayo yalituwezesha kuimarisha uhusiano kati yetu. Pamoja na mapambano yetu ya kila siku na watu wanaoishi katika umaskini, sasa tunashiriki katika changamoto mbili za muda mrefu. Katika uhalisia wake: nia ni kuelewa kwa undani maisha na mapambano ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri na kukusanya watu kutoka kila sehemu ya jamii na kuhakikisha lengo la mradi ni kwa wale wote wanaoishi katika umaskini uliokithiri.
Wanaharakati wa kujitolea wa ATD, na marafiki wa ATD wanaoishi katika umaskini na wasioishi katika umaskini wanahusika kusikiliza na kuelewa kile wanacho kieleza watu wanaoishi katika hali ya umaskini. Kisha wao watapendekeza watunga sera, kimataifa au kitaifa, wataalamu na wananchi katika kuzingatia uzoefu wa wale ambao hukabiliana na matatizo yaliokithiri.
Kufanikisha Elimu kwa Wote ni changamoto kubwa. Kama tulivyoelezea katika jarida lililopita, tunafanyakazi juu ya suala hili muhimu. Kamati inaundwa na wanachama wa ATD kutoka sehemu mbalimbali Tegeta, Tandale na Soko la Samaki la Dar es Salaam ambao wanafanya kazi hii. Rafiki yetu Selemani atazungumzia zaidi kuhusu hili kwenye ukurasa unaofuata.
Changamoto ya pili ni kutambua viashiria vipya vya umaskini katika mradi wa utafiti duniani kote. Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Oxford pendekezo limeandaliwa kwa benki ya dunia kufadhili mradi huu mkubwa. Miradi hii mara nyingi mno huwatenga watu wenye uzoefu wa kuishi katika hali ya umaskini uliokithiri. Itakuwa nafasi kwa ajili yetu, nchini Tanzania, ili kukuza sera mpya na kutafuta njia mpya ya kuelewa hali ya kutengwa kwa kupitia uzoefu wa wale wanaoishi kwenye hali hiyo.
Tuko katika hatua ya awali. Kila mtu anaweza kushiriki katika suala hili, Karibu sana!!
Salehe Seif Mwanaharakati kutoka katika tim,